Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaendesha mradi wa mafunzo kwa wanawake Bangladesh

UNHCR yaendesha mradi wa mafunzo kwa wanawake Bangladesh

Mradi wa kuwapa wanawake mafunzo ambao hawana uwezo wa kupata ajira uliofadhiliwa na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR umetajwa kuwa wenye manufaa kwa familia zao.

Kati ya mafunzo wanayopata wanawake hao ni kama ushonaji na mradi huo una lengo la kuwapa ujuzi mpya wanawake ambao wamekuwa wakifanya kazi za ushonaji vijijini mwao.

UNHCR ilianza kuhudumu katika eneo hilo mwaka 1994 ikiwa na lengo la kuwavutia wakimbizi waliokuwa wakiishi nchini Bangladesh kurudi nyumbani. Eneo hilo linalokabiliwa na uhaba wa raslimali na miundo mbinu duni ina maana kuwa wenyeji wana uwezo mdogo wa kuenda shuleni au kupata ajira.