Skip to main content

WFP yatumia dola milioni sita kuwasaidia Wakyrgystan mwaka huu

WFP yatumia dola milioni sita kuwasaidia Wakyrgystan mwaka huu

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa limetumia karibu dola milioni sita mwaka huu kuwasaidia watu 240,000 waliothirika na mizozo kusini mwa Kyrgzstan na wengine 340,000 katika mikoa sita kati ya mikoa saba nchini humo.

WFP inasema kuwa hiki ndicho kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na shirika hilo kwa mwaka mmoja pekee nchini Kyrgyzstan . Fedha hizo zilitumika kugharamia mahitaji kama chakula na usafirishaji wa bidhaa katika maeneo yaliyokuwa yameathirika na mizozo mwezi Aprili.

Mzozo wa mwezi Aprili uliomuondoka madarakani rais Kurmanbek Bakiyev sawia na ghasia za kikabila zilizoibuka kusini mwa Kyrgyzstan mwezi Juni vilisababisha maelfu ya watu kuhama makwao na kuwaacha wakiwa na mahitaji makubwa. WFP imehudumu nchini Kyrgyzstan tangu mwaka 2008 na mwaka huu imesambaza karibu tani 20,000 za chakula.