WFP umeongeza muda wa kusaidia mpango wa chakula nchini Bangladesh

30 Disemba 2010

Bodi ya wakurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP imeidhinisha kuongeza mwaka mmoja zaidi ya mpango wa msaada wa chakula nchini Bangladesh.

Mpango huo unawasaidia watu takribani milioni 2.1 wanaokabiliwa na njaa, wasiojiweza na wenye utapia mlo, na unagharimu dola milioni 76. Uamuzi huo utaiwezesha WFP kuendelea na mipango ya kupunguza utapia mlo na kuimarisha usalama wa chakula kwa watu masikini nchini Bangladesh hadi mwishoni mwa mwaka 2011.

Kwa mujibu wa WFP mpango huo sio tuu utaimarisha ushirikiano na serikali, bali utawasaidia Wabangladesh katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. George Njogopa na ripoti kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter