Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umelaani vikali shambulio la Bomu lililokatili maisha ya watu Helmand Afghanistan

UM umelaani vikali shambulio la Bomu lililokatili maisha ya watu Helmand Afghanistan

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa nchini Afghanistan Staffan De Mistura amelaani vikali shambulio la bomu lililotegwa barabarani hii leo na kulipua basi la abiria kwenye mji wa Hahr-s-Saraj wilaya ya Helmand.

Raia 14 wameuawa kwenye shambulio hilo na wengine wengi kujeruhiwa wakiwemo watoto. De Mistura ametoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwa ndugu na familia ya waliopoteza maisha. Amesema kutega mabomu barabarani kwa kuwalenga raia ni kinyume na sheria za kiamatifa na hakuna kinachoweza kuhalalila vitendo hivyo.

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA na timu ya wapigania haki za binadamu wanakusanya taarifa ili kupata chanzo cha tukio hilo.