Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa DR Congo waendelea kufurushwa Angola :UM

Wakimbizi wa DR Congo waendelea kufurushwa Angola :UM

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaotimuliwa kutoka nchi jirani ya Angola wanaendelea kuwasili nyumbani Congo, huku wengi wakiarifu kubughudhiwa ikiwa ni pamoja na kubakwa imesema ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu nchini humo OCHA.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo watu 1355 walitofukuzwa Angola wamewasili katika majimbo ya Bas-Congo na Kasai tangu tarehe 11 mwezi huu. Wimbi jipya la kurejea kwa wakimbizi hao linafanya idadi ya wakimbizi waliotimuliwa Angola tangu Septemba mwaka huu kufikia 12,000. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)