Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa Ache imepiga hatua bado kunachangamoto :UM

Ingawa Ache imepiga hatua bado kunachangamoto :UM

Chimbo la Ache nchini Indonesia limepiga hatua kubwa ya ujenzi mpya tangu kukumbwa na janga la tsunami miaka sita iliyopita. Hata hivyo ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kwamba bado linakabiliwa na changamoto kubwa ya kuondoa umasikini, kuleta usawa na athari za majanga kwa siku zijazo.

Ache moja ya maeneo yaliyoathirika vibaya zaidi katika nchi 11 zilizokubwa na tsunami katika bahari ya Hindi mwaka 2004 ambayo ilikatili maisha ya watu 230,000 na uharibifu wa mamilioni ya dola, imepiga hatua katika kukarabati miundombinu, huduma za jamii na kuwawezesha wanajamii katika sekta mbalimbali.

Hayo yamo kwenye ripoti ya kwanza kabisa ya maendeleo iliyotayarishwa na serikali kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP. Hata hivyo ripoti hiyo imesema changamoto kubwa iliyosalia ni kupunguza umasikini, kuimarisha usalama, kupunguza athari za majanga siku zijazo, kuwawezesha wanawake, kuleta usawa katika majimbo ambayo hayajaendelea

Ripoti hiyo imeongeza kwamba umri wa watu kuishi umeongezeka kwa mwaka mmoja kutoka miaka 67 hadi 68 tangu mwaka 2002, na hali ya umasikini imepungua na kufikia asilimia 22 kutoka asilimia 30 mwaka 2002, lakini bado iko juu ya asilimia 14 inayotakiwa kwa nchi nzima.