Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Lebanon aahidi ushirikiano zaidi kwa vikosi vya UM

Rais wa Lebanon aahidi ushirikiano zaidi kwa vikosi vya UM

Rais wa Lebanon amesema kuwa nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa ambavyo vilipelekwa nchini humo mwaka 2006 kufuatia makubaliano yaliyomaliza mapigano kati ya Israel na Hizbollah

Rais Michel Sleiman ambaye jana alitembelea makao makuu ya vikosi hivyo UNIFIL katika eneo Naqoura lililoko Kusini mwa nchi hiyo amehaidi kutoa uungwaji mkono wa dhati kwa vikosi hivyo.

Katika ziara yake hiyo rais huyo alimbatana na maafisa kadhaa wa jeshi na kisha kupewa maelezo toka kwa mwenyeji wao Major General Alberto Asarta Cuevas. Kamanda huyo wa vikosi vya umoja wa Mataifa ameita ziara ya rais Sleiman kama ushirikiano wa dhati ambaoLebanon inaashria kwa vikosi hivyo.