Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2010 umekuwa wa changamoto za kiafya:WHO

Mwaka 2010 umekuwa wa changamoto za kiafya:WHO

Shirika la afya duniani who limeutaja mwaka 2010 kama mwaka uliokuwa na changamoto nyingi za kiafya zikiwemo za majanga ya kiasili.

Hata hivyo WHO imeutaja mwaka 2010 kama mwaka ambapo kulishuhudiwa ushirikiano wa kukabalina na matatizo yanayolikummba bara la afrika. WHO inasema kuwa mapema mwaka huu kulitokea janga kubwa la tetemeko la ardhi nchini Haiti ambapo uliongoza mashirika mengine kutuo huduma nchini humo.

Baadaye kuliposhuhudiwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti WHO iliongoza huduma zingine kama hizo. Pia mwaka 2010 WHO ilitoa madawa na huduma za matibabu kwa karibu watu milioni 6.7 baada ya mafuriko kuikumba Pakistan.

Hata hivyo kulishuhudiwa hatua katika kutimizwa kwa malengo ya kiafya ya millennia . Pia ni mwaka huu ndipo kulitangazwa dawa mpya na nafuu ya kutibu ugonjwa wa uti wa mgongo ugonjwa unao hatarisha maisha ya zaidi ya watu milioni 450 barani afrika.