Mafuriko Australia yanaashiria umuhimu wa kujiandaa:UNISDR

Mafuriko Australia yanaashiria umuhimu wa kujiandaa:UNISDR

Mafuriko yanayoighubika Australia hivi sasa kwa mara nyingine yanaashiria umuhimu wa nchi zote zinazoendelea na zilizoendelea kuwa na mipango imara au la kukabiliwa na athari kubwa za hali ya hewa limesema shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kupunguza majanga UNISDR.

Mvua kubwa zimesababisha eneo la Kaskazini Mashariki mwa Australia likiwa kufurika, na miji na vijiji katika jimbo la Queensland na New South Wales kutangazwa kama maeneo ya hatari ya majanga. Mamia ya watu katika eneo hilo wamelazimika kuondka huku wengine wakihamishwa kwa kutumia helkopta.

Mafuriko hayo pia yameharibu kabisa mazao kama ngano na pamba na kuathiri shughuli za mgodi wa makaa ya mawe wa Queensland. Duru zinasema athari za mafuriko hayo zinaweza kufikia dola bilioni moja.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataia wa UNISDR Margareta Whalstrom anasema endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa na nchi zote duniani basi gharama kama hizo zitakuwa si jambo jipya bali ni kitu cha kawaida.