Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO imezindua mchezo kwenye wavuti kuelimisha vijana kuhusu Ukimwi

UNESCO imezindua mchezo kwenye wavuti kuelimisha vijana kuhusu Ukimwi

Umoja wa Mataifa umezindua mchezo wa video kwa kutumia wavuti kwa lengo la kuwapa vijana taarifa muhimu kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV, huku ukiwaelimisha, kuwaburudisha na kuchagiza tabia njema zinazojali afya zao.

Mchezo huo wa computer uitwao "Fast Car" safari salama duniani kote umezinduliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni ukiwalenga vijana wa zaidi ya umri wa miaka 16. Na mchezo huo umetafsiriwa katika lugha za Kiingereza, Kifaransa na Kirusi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

 

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

Watakaoshiriki kwenye michezo kwenye mabara matano tofauti watakuwa na fursa ya kuingia kwenye maeneo ya kitamaduni ya shirika la UNESCO na kupata habari kuhusu njia za kujikinga na matibabu ya ugonjwa ya ukimwi.

Michezo hii una lengo la kuwahamasisha vijana kuhusu ugonjwa wa ukimwi na kuwafanya kuelewa mbinu na njia za kujikinga kutoka kwa maradhi hayo. UNESCO inasema kuwa masuala yanayayohusiana na ugonjwa wa ukimwi mara nyingi huwa vigumu kuzungumzwa moja kwa moja kwa watoto na hata kwa watu wazima.

Mara nyingi wazazi uona haya au hukosa habari mwafaka kuhusu ugonjwa wa ukimwi na pia hawana ujuzi wa kutosha kuzungumza na watoto kuhusu njia za kujikinga kutokana na maradi ya ukimwi. Inakadiriwa kuwa karibu vijana 3,500 wanaambukizwa ugonjwa wa ukimwi kila siku kote duniani na wengi wao hawana uwezo wa kupata habari kuhusu ugonjwa huo.