Kipindupindu kuathiri mavuno ya mpunga Haiti: FAO

29 Disemba 2010

Sehemu kubwa ya mavuno ya mpunga Kaskazini Magharibi mwa Haiti yatapotea kwa sababu wakulima wanahofia ugonjwa wa kipindupindu kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO.

Ripoti ya shirika hilo inaonyesha kwamba wakulima wengi wanakwepa mavuno wakihofu kwamba maji katika mito na mifereji ambayo humwagilia mpunga na mashamba mengine yanaweza kuwa na vidudu vya kipindupindu. Wanunuzi pia wamearifiwa kutokuwa tayari kununua mazao kutoka katika eneo hilo ambalo limeathirika la kipindupindu, hali ambayo itaathiri zaidi sekta ya kilimo nchini humo.

FAO inasema inafanya kazi kwa karibu na serikali ya Haiti na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na afya na usafi kuwapa wakulima taarifa sahihi kuhusu hatua za tahadhari za kuchukua wakiwa shambani.

Kwa mujibu wa Annika Kaipola mratibu wa masuala ya dharura wa FAO mjini Roma, ni muhimu sana kwa hatua za kuzuia magonjwa kuchukuliwa hususani na jamii ya wakulima.

(SAUTI YA ANNIKA KAIPOLA)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter