Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kundi la watu wenye hasira washambulia UNOCI Ivory Coast

Kundi la watu wenye hasira washambulia UNOCI Ivory Coast

Umati wa watu wenye hasira wameshambulia msafara wa walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI hii leo nje kidogo ya mji wa Abijan.

Shambulio hilo limetokea wakati mkuu wa masuala ya kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Alain Le Roy akizuru nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.Ivory Coast inakabiliwa na mvutano wa kisiasa ambapo Rais Laurent Gbagbo aliyeshindwa uchaguzi amegoma kumwachia Alassane Ouattara kushika hatamu kama rais anayetambuliwa kushinda uchaguzi.

Msemaji wa UNOCI Hamadoun Toure amesema mpango wa UM unaendelea kutekeleza wajibu wake ingawa wakati mwingine wanakabiliwa na vikwazo vingi. Amesema mfano leo msafara wao umeshambuliwa na watu wenye hasira , gari lao moja kuchomwa moto na askari mmoja mlinda amani kujeruhiwa kwa mapanga.