Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Familia 42,00 zasitishiwa msaada wa chakula Pakistan

Familia 42,00 zasitishiwa msaada wa chakula Pakistan

Msaada wa chakula kwa familia 42,000 kwenye jimbo la Bajaur nchini Pakistan umesitishwa na mpango wa chakula duniani WFP kufuatia shambulio la kujitoa muhanga siku ya Jumamosi.

Shambulio la kujitoa muhanga lilikatili maisha ya watu 45 kwenye kituo cha polisi cha ukaguzi karibu na kituo cha kugawia chakula kinachoendeshwa na WFP mjini Khar. Kwa mujibu wa msemaji wa WFP Amjad Jamal kusitishwa huko ni kwa muda na pindi hali ya usalama itakapotengamaa ugawaji utaanza tena kama kawaida.

WFP inagawa chakula kwa familia 42,000 kwa mgao wa kila mwezi, na ni mchanganyiko wa unga wa ngano, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi, biskuti kwa ajili ya watoto na chakula ambacho kiko tayari kwa ajili ya watoto wachanga.