Skip to main content

Serikali za Afrika zaweza kuwa chachu ya uchumi:UM

Serikali za Afrika zaweza kuwa chachu ya uchumi:UM

Serikali za Afrika zinaweza kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo endelevu kupitia sera ambazo zitatoa mikopo kwa biashara na viwanda ili kuenendelea.

Hayo yame kwenye tathimini ya ripoti ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika ilitotolewa leo. Ripoti hiyo ya kila mwaka ya mtazamo wa uchumi kwa Afrika ERA inayotolewa na tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika ECA na muungano wa Afrika AU imeangalia rekodi ya mataifa katika kuchagiza maendeleo barani Afrika na kutoa mifano hai ya mafanikio kutoka barani humo na kwingineko.

Pia imependekeza kuchukuliwa hatua za kuchagiza uchumi na maendeleo. Ushahidi kutoka Asia na nchi zingine zilizoendelea unatoa mtazamo wa haja ya kujikita katika jukumu la serikali kudhibiti maendeleo.

Mswada wa ripoti hiyo ulipitiwa na wataalamu kutoka taasisi zenye kuheshimiwa duniani walikusanyika mjini Addis Ababa ambako ndio makao makuu ya ECA na AU. Wataalamu hao wamesema wakati uchumi wa Afrika unakuwa unahitaji mabadiliko makubwa ili kuwafaidi watu wake.