Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaendelea kutoa msaada kwa ajili ya kuara ya maoni ya kihistoria ya hatma ya Sudan Kusini

UM unaendelea kutoa msaada kwa ajili ya kuara ya maoni ya kihistoria ya hatma ya Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umewasilisha makaratasi ya kupigia kura kwa watu zaidi ya milioni 4 Kusini mwa Sudan.

Kura ya maoni ya kuamua endapo eneo hilo la Kusini lijitenge na kuwa taifa huru ama la inatarajiwa mapema mwezi Januari kukamilisha machakato wa amani uliomaliza miongo miwili ya vita kati ya Kusini na Kaskazini. Kila karatasi ya kupigia kura ina picha mbili, mkono mmoja unaoashiria uhuru, na mikono miwili inayomaanisha umoja.

Hali mbaya ya hewa barani Ulaya ilitishia kuchelewesha kuwasili kwa karatasi hizo zilizochapishwa nchini Uingereza , kwa ajili ya kura ya tarehe 9 hadi 15 Januari, lakini ziliwsili kwa wakati Juba mji mkuu wa Sudan Kusini wiki iliyopita .

Masanduku hayo ya karatasi za kupigia kura yaliwasilishwa na mpango maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kura ya maoni na kitengo cha uchaguzi UNIRED ulioungdwa kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP na mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa Sudan UNMIS.

Karatasi hizo pia ziliwasilishwa mjini Khartoum kwa ajili ya Wasudan Kusini wanaoishi eneo la Kaskazini.

Mbali ya karatasi za kupigia kura UNDP pia imesaidia kuunda vituo vipatavyo 3000 kwa kupigia kura na kuwaandikisha mamilioni ya watu Sudan na katika nchi nyingine nane.