Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano na Paul Kagwa kuhusu homa ya manjano Uganda

Mahojiano na Paul Kagwa kuhusu homa ya manjano Uganda

Mlipuko mya wa homa ya manjano nchini Uganda umekatili maisha ya watu 45 hadi sasa na wengine zzaidi ya 100 wameathirika.

Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo wilya kumi za Kaskazini mwa Uganda zimeathirika na watu 183 wamethibitika kuambukizwa homa hiyo inayosambazwa na mbu.

Shirika la afya duniani WHO, shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF, shirika la Marekani la msaada USAID na wizara ya afya ya Uganda wako katika mkakati kabambe wa kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo na kutoa chanjo na tiba kwa waathirika.

Kupata ufafanuzi zaidi wa ukubwa wa mlipuko huo ambayo mara ya mwisho ulizuka miaka 1950 Flora Nducha amezungumza na msemaji wa wizara ya afya ya Uganda Dr Paul Kagwa.