Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupunguza unyanyapaa na kuelimisha ni muhimu katika vita vya ukimwi Sri Lanka:UNAIDS

Kupunguza unyanyapaa na kuelimisha ni muhimu katika vita vya ukimwi Sri Lanka:UNAIDS

Kupunguza unyanyapaa na kuelimisha jamii kunahitajika ili kudhibiti na kuzuia kusambaa kwa virusi vya ukimwi nchini Sri Lanka.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS elimu ya maambukizi ya ukimwi ni ndogo nchini humo, huku takwimu za karibuni za serikali zikionyesha kuwa kwa Desemba mwaka 2009 kulikuwa na visa 1196 ambavyo ni chini ya asilimia 0.1 miongoni mwa watu wa umri wa miaka kati ya 15 na 49 na chini ya asilimia moja kwa kundi lililokatika hatari ya kuambukizwa takwimu zinazoonyesha maambukizi ni madogo sana nchini humo.

Hata hivyo thatmini sahihi ya maambukizi ya HIV ni vigumu kuipata hasa kutokana na unyanyapaa na ukosefu wa eklimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huo, hususani kuzuia na taarifa za kampeni ni ngumu kuzipata.

UNAIDS inakadiria kwamba idadi ya maambukizi ni mara tatu zaidi ya takwimu rasmi za serikali na juhudi za kuelimisha jamii kuhusu ukiwmi zinakabiliwa na upinzani mkubwa, na unyanyapaa umewafanya waathirika wengi kutojitokeza , kupimwa au kuelezea hali yao ya afya.

Haya yamo kwenye ripoti ya pamoja ya UNAIDS na jumuiya ya uzazi wa mpango nchini humo, ambayo pia imeonya kuwa ni vigumu kuanzisha program za kuwasaidia wanoishi na virusi vya ukiwmi.