Rais Bashir kukubali matokeo ya kura ya maoni Sudan Kusini

28 Disemba 2010

Rais Omar Al Bashir wa Sudan amesema atakubali uamuzi wowote utakaofanywa na watu wa Sudan Kusini katika kura ya maoni ya kuamua endapo eneo hilo lijitenge na kuwa taifa huru ama la hapo Januari 9.

Bashir amesema Sudan Kaskazini itatoa msaada utakaohitajika na Sudan Kusini kama wataamua kujitenga na kuwa taifa huru au la. Rais Bashir ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Al-Jazira katikati mwa Sudan. Ameongeza kuwa serikali ya Sudan itawasaidia watu wa Kusini kuijenga nchi yao kwa vile anataka taifa hilo liweze kujimudu bila matatizo. Mapema mwezi huu Rais huyo alisema eneo la Kaskazini ambalo lina Waislamu wengi baada ya kura ya maoni litadumisha sheria za Kiislam au sharia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter