Mlipuko wa homa ya manjano wauwa watu zaidi ya 40 Nchini Uganda

28 Disemba 2010

Shirika la afya duniani WHO linaisaidia wizara ya afya ya Uganda kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano ambao umeshakatili maisha ya watu zaidi ya 40.

Mlipuko huo umeathiri wilaya nyingo za Kaskazini mwa Uganda na serikali imetenga vituo maalumu katika wilaya zilizoathirika. Chanjo hivi sasa inapelekwa katika wilaya hizo na WHO.

(SAUTI YA PAUL KAGWA)

Watu walianza kuumwa mwezi mmoja uliopita na kwa mujibu wa afisa wa afya katika wilaya ya Kitgum miongoni mwa zilizoathirika ni tarehe 24 Desemba siku ya mkesha wa Krismasi ndio ilithibitika kuwa ugonjwa huo ni homa ya manjano. Jason Nyakundi ya ripoti kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter