Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa ECOWAS wawasili nchini Ivory Coast

Ujumbe wa ECOWAS wawasili nchini Ivory Coast

Marais watatu kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Magharibi ECOWAS wamewasili mjini Abijan Ivory Coast kumshawishi Rais Laurent Gbagbo kukubali kushindwa na kuondoka madarakani.

Marais hao Yayi Boni wa Benin, Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone na Pedro Pires wa Cape Verde watamshawishi Gbagbo kukabithi madaraka kwa bwana Alassane Ouattara ambaye anakubalika na kutambuliwa kama mshindi halali wa uchaguzi wa mwezi uliopita.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kulinda amani Alain Le Roy aliwasili jana nchini Ivory Coast na kufanya mazungumzo na Bwana Ouattara ambaye kwa sasa makao yake makuu yanalindwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI. Taarifa kamili na George Njogopa.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Naye msemaji wa UNOCI nchini Ivory Coast Hamadoun Toure akifafanua kuhusu wajibu wao amesema

(SAUTI YA HAMADOUN TOURE)