Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia zilizosababisha maafa Nigeria zalaaniwa na Ban

Ghasia zilizosababisha maafa Nigeria zalaaniwa na Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani ghasia zilizoshuhudiwa katika sehemu kadha nchini Nigeria katika siku za hivi maajuzi na kusababisha vifo vya watu 30 huku wengine zaidi ya 70 wakijeruhiwa.

Kulishuhudiwa mashambulizi ya mabomu katika mji wa Jos katika jimbo la Plateau siku ya Ijumaa na kufuatiwa na makabiliano makali mjini humo mji ambao umekuwa ukikumbwa na ghasia awali kati ya waumini wa kikirsto na wa kislamu.

Wakati wa ghasia hizo kundi moja la kiislamu lilishambulia makanisa mawili katika jimbo la kaskazini la Borno ambapo watu kadha waliuawa. Kupitia kwa msemaji wake Ban alishutumu mashambulizi hayo hususan wakati huu mamilioni ya watu wanaposherehekea sherehe takatifu ambapo pia aliiunga mkono jitihada za serikali ya Nigeria za kuwachukulia hatua wahusika.