Skip to main content

Ban alaani shambulio la kigaidi Pakistan

Ban alaani shambulio la kigaidi Pakistan

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani shambulizi la kigaidi lililotekelezwa nje ya kituo cha kusambaza misaada cha shirika la mpango wa chakula duniani WFP mashariki kwa Pakistan ambalo lilisababisha watu 45 na kuwajeruhi wengine wengi.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa mshambuliaji wa kike wa kujitoa mhanga alitekeleza shambulizi kwa umati wa watu uliokuwa ukipokea msaada wa chakula katika eneo la Khar. Kupitia kwa Msemaji wake Ban alituma risala zake za rambi rambi kwa familia za waliouawa kwenye shambulizi hilo, kwa serikali na kwa watu wa Pakistan.

Ban amesema kuwa hata baada ya kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa usalama likiwemo shambulizi kwenye kituo cha WFP mwaka 2009 . Shirika hilo bado linaendelea kuwasaidia karibu watu milioni kumi mwaka huu.