Rais wa baraza kuu la UM amesema maendeleo na utawala wa kimataifa ni ajenda zilizotawala baraza mwaka huu

Rais wa baraza kuu la UM amesema maendeleo na utawala wa kimataifa ni ajenda zilizotawala baraza mwaka huu

Wakati kikao cha 65 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikikunja jamvi, rais wa baraza hilo Joseph Deiss amepongeza mkutano huo ambao amesema ulifungua njia ya kuongeza kasi ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa na kuondokana na umasikini na maradhi yanayoisumbua dunia.

Bwana Deiss amesema maendeleo na utawala wa kimataifa zimekuwa ajenda kubwa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa na kutoa tathimini ya mwaka 2010 deis amesema moja ya mambo muhimu kwa mwaka huu ni mkutno huo uliofanyika hapa New york na kuhudhuriwa na wakuu wa nchi zaidi ya 100 ambao wamesisitiza kwamba malengo ya maendeleo ya milenia ili kuboresha maisha ya watu lazima yafikiwe ifikapo 2015.Bwana Deiss amesema suala la utawala wa kimataifa ni vigumu kuelewa lakini dunia inabadilika.

(SAUTI YA JOSEPH DEISS)

"Tunakabiliwa na matatizo zaidi na zaidi ambayo hayawezi kutatuliwa na taifa moja moja. Na kwa upande mwingine mataifa yote yanataka kuwa huru, hivyo jinsi gani tutaweza kuyaleta mataifa yote haya pamoja na kutatua matatizo kama ongezeko la joto duniani, lakini pia kwa lugha nyepezi naweza kusema jukumu kubwa la Umoja wa Mataifa ambalo ni amani kwa dunia nzima au matatizo mengine kama uhamiaji, ugaidi na mengineyo.