Mkataba kufuatilia kupotea kwa watu waanza kutekelezwa leo: UM

23 Disemba 2010

Mkataba muhimu wa kufuatilia kupotea kiholela au kwa lazima kwa watu unaanza kutekelezwa leo huku wataalamu wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kuzisaidia familia kujua hatma ya wapi waliko jamaa zao waliopotea, wameyataka mataifa yote kuhakikisha wanakomesha uhalifu huo kwa kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.

Mkataba wa kimataifa wa kuwalinda watu wote kutokana na kupotea kiholela au kwa lazima ambao ulipitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa 2006 unaanza kutekelezwa siku 30 baada ya Iraq kuwa taifa la 20 kutia saini.

Katika taarifa maalumu, watalaamu hao wamesema kuanza kutekelezwa kwa mkataba huo ni hatua muhimu kuelekea kunakotakiwa lakini haitoshi ,wametaka kila nchi kufanya juhudi za kuzuia na kukomesha hali hiyo.

Kupotea kiholela au kwa lazima kunamaanisha , kukamatwa, kuwekwa mahabusu, kutekwa na mifumo mingine ya kunyimwa haki na uhuru kunakofanywa na vibaraka wa mashirika au serikali, watu binafsi, au makundi ya watu, kwa msaada na idhini ya serikali.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter