Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi imepiga hatua kubwa katika kuboresha afya ya uzazi

Burundi imepiga hatua kubwa katika kuboresha afya ya uzazi

Ni miaka isiyozidi mitano iliyosalia kabla ya 2015 muda ambao ni kikomo cha utekelezaji wa malengo yote manane ya maendeleo ya milenia yaliyoafikiwa na viongozi wa dunia mwaka 2000. Burundi ikiwa ni mmoja wa wao

Na kwa sasa nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika moja ya malengo hayo linalojikita katika upatikanaji wa huduma bora za afya ya uzazi. Hii ni baada ya serikali ya nchi hiyo kuazimia kuhakikisha kina mama wanajifungua pasi na malipo na hivo kuwachagiza wengi kwenda kujifungulia hospitali katika mazingira ya huduma bora .

Huku malengo ya milenia yakiagiza kupunguza robo tatu idadi ya vifo vya uzazi ifikapo mwaka 2015, maafisa wa Burundi wanasema pamoja na changamoto kadhaa, dalili zote zinaonyesha kwamba watakuwa karibu kufikia lengo hilo.

Hata hivo changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni ongezeko la idadi ya watu nchini humo. Mwandishi wetu mjini Bujumbura Ramadhani Kibuga anatathimini hali ilivyo katika makala hii.