Wakati kura ya maoni ikikaribia Sudan Kusini jopo la UM limezitaka pande zote kuhakikisha inakuwa huru

22 Disemba 2010

Mkuu wa jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia kura ya maoni ya mwezi ujao ya kuamua kujitenga ama la kwa Sudan Kusini amesema timu yake inaamini kwamba kura itafanyika kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizosalia ikiwa ni pamoja na ukosefua wa fedha na elimu kwa wapiga kura.

Akizungumza mjini Khartoum na waandishi wa habari hii leo baada ya kumaliza ziara yao ya tatu mwenyekiti wa jopo hilo Benjamin Mkapa Rais wa zamani wa Tanzania amesema kutokana na waliyoyashuhudia wanaimani kura ya maoni itafanyika kama ilivyokusudiwa.

Rais wa Sudan Kusini watapiga kura tarehe 9 hadi 15 Januari kuamua endapo wajitenge na kuwa taifa huru. Kura hiyo ya maoni ni itakuwa ni utekelezaji wa moja ya vipengele vya makubaliano ya amani ya CPA yaliyitiwa saini 2005 na kumaliza miongo miwili ya vita baina ya Kaskazini na Kusini.

Uandikishaji wapiga kura kwa mujibu wa Mkapa umemalizika na mahaka itasikiliza changamoto zilizopo kabla ya kutolewa orodha ya mwisho ya wapiga kura. Kura hiyo ya maoni itafanyika sanjari na ile ya jimbo la Abyei lenye utajiri wa mafuta ambalo litaamua lisalie upande wa Kaskazini au Kusini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter