Mashirika ya misaada yasaidie wakimbizi wa Colombia:UNHCR

Mashirika ya misaada yasaidie wakimbizi wa Colombia:UNHCR

Colombia na Ecuador zinatoa wito kwa mashirika ya kimatifa kubuni mpango wa kuwasaidia zaidi ya wakimbizi 52,000 kutoka Colombia wanaoishi nchini Ecuador.

Shirika la uhamiaji la kimataifa IOM limekuwa likishiriki kwenye miradi katika eneo la kaskazini mwa mpaka wa Ecuador ya kuwasaidia wakimbizi wa Colombia na wenyeji wengine wa Ecuador. Msemaji wa IOM Jared Bloch anasema kuwa shirika lake litashirikiana na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR katika mpango wa kuwasaidia wakimbizi hao.

Mpango huo pia unahusika katika kuwasaidia wakimbizi wanaorejea nyumbani na pia kuinua maisha ya wanaosalia hususan katika sekta za afya , makao na elimu.