Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 25 tuu ya msaada wa kipindupindu Haiti ndio umepatikana: UM

Asilimia 25 tuu ya msaada wa kipindupindu Haiti ndio umepatikana: UM

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema tatizo la kipindupindu Haiti halijamalizika huku msaada ulioombwa kukabiliana na ugonjwa huo umepatikana asilimia 25 tuu.

Kwa mujibu wa mkuu wa OCHA Valarie Amos kati ya dola bilioni 174 zinazohitajika kukabiliana na ugonjwa huo ni dola milioni 44 tuu ndio zilizopokelewa hadi sasa, na mbali ya hayo mwaka 2010 umekuwa mgumu sana kwa Wahaiti waliokumbwa na tetemeko, kimbunga na sasa ugonjwa.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

Watu zaidi ya 2000 wamefariki dunia kwa kipindupindu chini Haiti huku wengine 60,644 wakilazwa hospitali. OCHA inasema kuna upungufu mkubwa wa magari ya kubebeba wagonjwa kuwapeleka kwenye vituo vya tiba.