Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ivory Coast inatia iko katika hatihati ya vita tena:UM

Ivory Coast inatia iko katika hatihati ya vita tena:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonya kwamba kuna hatari kubwa ya kurejea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast.

Tamko hilo limefuatia hali ya mvutano wa kisiasa unaondelea nchini humo baada ya Rais Laurent Gbagbo aliyeshindwa uchaguzi kugoma kuondoka madarakani. Gbagbo amevitaka vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI na vya Ufaransa kuondoka nchini jambo ambalo Umoja wa Mataifa umelipinga.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini Ivory Coast Y.J.Choi leo ameielezea hali nchini humo kama mchezo wa paka na panya wenye hatari kubwa kwa mamilioni ya raia. Ufaransa imewaonya raia wake walioko nchini humo kuchukua tahadhari na hasa kuondoka.

Naye mkuu wa masula ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa Alain Le Roy amemtaka Bwana Gbagbo na wafuasi wake kutowachokoza walinda amani wa Umoja wa Mataifa na kukiuka haki za binadamu.

(SAUTI YA ALAIN LE ROY)

Nayo Bank ya dunia imetangaza kuwa inasitisha mikopo yote kwa Ivory Coast kutokana na hali inayoendelea.