Serikali mpya ya Iraq ni hatua kubwa katika demokrasia:Ban

Serikali mpya ya Iraq ni hatua kubwa katika demokrasia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekaribishwa kutangazwa kwa serikali mpya mjini Baghdad na kusema ni hatua kubwa kuelekea mchakato wa demokrasia nchini Iraq.

Ban ameitaka serikali hiyo mpya sasa kutoa umuhimu kwenye maridhiano ya kitaifa, ujenzi mpya na utulivu na amani ya kudumu. Ban ambaye amekuta akitoa wito wa kuwa na serikali ya kudumu tangu kufanyika kwa uchaguzi mwezi Machi, amewapongeza viongozi wa kisiasa wa Iraq kwa juhudi zao za kuhakikisha kwamba serikali mpya inajumuisha pande zote na kuungwa mkono na Wairaq wote.

Katika taarifa maalumu amewataka washirikiane katika umoja wa kitaifa ili kukamilisha kwa amani mchakato wa kuundwa kwa serikali na kushughulikia changamoto kubwa zinazoikabili nchi hiyo. Katibu Mkuu ameahidi kuendeleza msaada kwa taifa hilo kutoka kwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada nchini Iraq UNAMI, kwa watu wa Iraq na serikali yao ili kujenga taifa la Iraq lenye matumaini na amani.