Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana waongoza ajenda kwenye mkutano wa baraza la usalama la UM

Vijana waongoza ajenda kwenye mkutano wa baraza la usalama la UM

Vijana kutoka kote duniani wameelezea mtazamo wao kuhusu masuala wanayoayona kuwa muhimu kwenye mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York leo.

Masuala hayo ni kuanzia uzalishaji wa nyuklia, vita, kutovumiliana, ugaidi, mazingira hadi amani na usalama wa dunia.  Baraza la usalama limepokea mawzo hayo kutoka kwa vijana wengi kwa kutumia mawasiliano ya njia ya video yaliyotumwa kwenye You Tube, Facebook au barua pepe.

Rais wa baraza la usalama mwezi huu balozi Susan Rice amesema mawazo mengi waliyopokea yameletwa kwa njia ya barua pepe lakini kulichaguliwa video tatu zilizochezwa kwenye mjadala huo leo.

(SAUTI YA SUSAN RICE)

"Video hizi zimewasilisha sauti kutoka katika maeneo matatu tofauti duniani, lakini kwa pamoja zimekusia mada ambazo tumezisikia kutoka katika mawazo mengi tuliyopokea. Kwa kifupi vijana wanataka amani, wanataka kulindwa kutokana na vita na umwagikaji wa damu. Wanaogopa kuhusu mazingira ambayo yatachochea vita na wanaoona uhusiano uliopo baina ya usalama na maendeleo."

Baraza la usalama liliandaa mkusanyiko wa maoni hayo yaliyowasilishwa na vijana ili yachezwe mwisho wa mdahalo huo.