Bangladesh na IOM kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

21 Disemba 2010

Bangladesh mbioni kuanzisha sheria ya kukabiliana na biashara ya usafirishaji haramu wa binadamuBangladesh imeanzisha kipengele cha awali cha sheria yenye lengo la kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Katika mpango huo mpya, Wizara ya mambo ya ndani inashirikiana na mashirika kadhaa ya kirai kwa ajili ya kuandaa sheria ambayo itatumika kuwabana wahusika wa biashara hiyo. Tayari mkakati huo umewasilishwa kwa shirika la uhamiaji la umoja wa mataifa ambalo linatazamia kutoa mchango mkubwa kufanikisha sheria hiyo.

Vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu vimekuwa vikiongezeka kila mara nchini Bangladesh. Wengi wanaotumbukia kwenye hali hiyo ni wale wanaozamia katika nchi za majuu kwa ajili ya kusaka ajira. Mwaka jana 2009 pekeee watu zaidi 900,000 waliondoka nchini humo kwenda nchi za nje kwa shabaya ya kusaka kazi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter