Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baridi kali iliyoikumba Ulaya kupungua kidogo: WMO

Baridi kali iliyoikumba Ulaya kupungua kidogo: WMO

Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kwamba hali ya baridi kupindulia inayoathiri sehemu za Ulaya Magharibi na Mashariki mwa Marekani itapungua katika siku chache zijazo.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO ingawa baridi kali sio kitu kigeni kwa majira kama haya ni vigumu kutabiri hali hii ya hewa ya kupindukia itaendelea kwa muda gani. Maelfu ya wasafiri wamekwama katika viwanja mbalimbali vya ndege barani Ulaya ambao barabu inayomwagika kwa wingi imeathiri usafiri katika kipindi ambacho kila mwaka kinakuwa na kinapilika nyingi. Claire Nullis ni afisa katika shirika la WMO.

(SAUTI YA CLAIRE NULLIS)

WMO inasema hali mbaya ya hewa kama hii ilishuhudiwa pia mwaka 2009, hata hivyo limesema si kawaida kushuhudia tukio hilo katika miaka miwili mfululizo.