Skip to main content

Mkuu wa haki za binadamu alaani ghasia nchini Belarus

Mkuu wa haki za binadamu alaani ghasia nchini Belarus

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea hofu yake juu ya ghasia na kuwekwa rumande kwa wagombea wa upinzani na wafuasi wao baada ya uchaguzi wa Rais uliofanyika Jumapili iliyopita nchini Belarus.

Pillay amelaani vikali machafuko na hali hiyo na ametoa wito kukomesha ghasia. Amesisitiza kwamba uongozi wa nchi hiyo ni lazima uheshimu na kuhakikisha haki za binadamu zinafuatwa dhidi ya wapinzani wao wa kisiasa , haki za maandamano ya amani na uhuru wa kuongea. George Njogopa na ripoti kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)