Skip to main content

UNHCR kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Ivory Coast

UNHCR kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa Ivory Coast

Taarifa kutoka nchini Ivory Coast zinasema majeshi yanayomuunga mkono Rais Laurent Gbabgo aliyeshindwa uchaguzi yameweka vizuizi kwenye Golf Hotel ambayo inatumiwa kama makao makuu ya muda ya bwana Alassane Ouattara alioyetangazwa kushinda uchaguzi wa Urais wa mwezi jana.

Vizuizi hivyo zinamaanisha msaada muhimu kama madawa na chakula haviwezi kuingia kwenye hoteli hiyo. Wakati huohuo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeimarisha maandalizi kusaidia ya uwezekano wa wimbi kubwa la wakimbizi.

Shirika hilo linasema limesafirisha msaada wa vitu muhimu kama chakula kwenye Liberia na Guinea ambako maelfu ya Waivory Coast wamekimbilia kuhofia usalama wao na kama anavyosema msemaji wa UNHCR Adrian Edwards wanajitayarisha kuwasaidia wakimbizi wapatao 30,000.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)