Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa lazima yatekeleze makubaliano ya Cancun:Figueres

Mataifa lazima yatekeleze makubaliano ya Cancun:Figueres

Mkuu wa masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito kwa nchi kuchukua hatua kufuatia makubalino ya karibuni ya mkutano wa Cancun ya kukata kwa kiasi kikubwa gesi chafu na kuzindua taasisi mpya na fedha.

Makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano uliomalizika Desemba 11 ni pamoja na kuzihalalisha rasmi ahadi na kuahkikisha zinatekelezwa, pamoja na kuchukua hatua madhubuti kupambana na ukataji miti ambao unachangia karibu 1/5 ya gesi cha cabon duniani.

Mkuu huyo Christina Figueres amesema mkutano wa Cancun ulikuwa hatua kubwa kuliko wengi walivyotarajia, lakini muda umewadia kwa wote kudhidi wamatarajio yetu kwa sababu chini ya hapo hakuna mafanikio.

Amesisitiza kwamba makubaliano ya Cancun yanahitaji kutekelezwa haraka iwezekanavyo na yaambatane na mfumo ambao utasaidia kupima mafanikio. Amesema nchi zote zinatakiwa kupunguza gesi za viwandani lakini zaidi mataifa yaliyoendelea kiviwanda na yafanye hivyo haraka.