Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa dawa za wadudu unasaidia kilimo Afrika Magharibi:FAO

Udhibiti wa dawa za wadudu unasaidia kilimo Afrika Magharibi:FAO

Wakulima wa Afrika Magharibi wamefanikiwa kupunguza matumizi ya dawa za kuulia wadudu , kuongeza uzalishaji, kuinua kipato na kuboresha mfumo wa kilimo kutokana na mradi wa kimataifa unaochagiza kilimo endelevu.

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO wakulima wapatao laki moja nchini Benin, Burkina Faso, Mali na Senegal wanashiriki katika mpango maalumu wa mafunzo ya jamii kuhusu kilimo na udhibiti wa matumizi ya dawa za kuulia wadudu yanayoendeshwa na FAo. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Wakifanya kazi kwa vikundi wakulima wadogo wanatumia mbinu bora za kilimo kujifunza na kufanya majaribio shambani. Mradi wa IPPM unasaidia katika kuboresha udongo pamoja na kutoa mafunzo kuhusu njia tofauti za kukabilina na wadudu waharibifu bila kutumia madawa ya kemikali. Pia mafunzo kuhusu kupata soko la mazoa ni moja ya mafunzo yanayotolewa.

Afisa wa kiufundi katika shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO William Settle anasema kuwa mifumo ya kilimo ambayo imekuwa ikitumika kwenye nchi za afrika magharibi imeambatana na matumizi ya madawa yenye athari kubwa. Amesema kuwa hali hii imesababishwa na kutoelewa athari zinazotoka na madawa ya kuua wadudu waharibifu, uchumi, afya na pia kwa jamii.