Baraza la usalama lashindwa kuafikiana kuhusu Korea Kaskazini

20 Disemba 2010

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuafikiana kuhusu tamko la msimamo wa hali ya mvutano inayoendelea Korea.

Korea ya Kusini Jumatatu ya leo imeendesha zoezi la kijeshi kwenye kisiwa cha Yeonpyong ambacho kilishambuliwa kwa mabomu na Korea ya Kaskazini Novemba 23. Kwa ombi la Urusi baraza la usalama limefanya mkutano wa dharura jana Juma[ili lakini baada ya saa nane za majadiliano halikuweza kuafikiana kutoa tamko la pamoja la kulaani mashambulizi ya Korea Kaskazini.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Rais wa mwezi huu wa baraza hilo Bi Susan Rice amesema

(SAUTI YA SUSAN RICE)

"Wajumbe wengi wa baraza la usalama wameweka bayana msimamo wao kwamba ni muhimu kulaani tukio la Novemba 23 na mashambulizi ya DPRK kwenye kisiwa cha Yeonpyong, lakini mtazamo huo haukufikia muafaka na wakati tukisubiri maelekezo muhimu kutoka katika kila mji mkuu, nadhani ni salama kutabiri kwamba mapengo yalilyopo sidhani kama yatazibwa."

Mapema mwaka huu Korea ya Kaskazini ililaumiwa kwa kuzamisha meli ya kivita ya Korea Kusini ya Cheonan ambapo mabaharia 46 waliuawa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter