Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya mpito ya nchini Somalia inaanza kudhibiti Mji Mkuu Mogadishu

Serikali ya mpito ya nchini Somalia inaanza kudhibiti Mji Mkuu Mogadishu

Serikali ya mpito inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Somalia inajiandaa kuchukua udhibiti wa nchini nzima kufutia wanamgambo wa Al Shabaab kuzidiwa nguvu na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini humo AMISOM.

Serikali ya mpito inasema hivi sasa inadhibiti zaidi ya nusu ya eneo lote la mji mkuu Moghadishu ambalo lilikuwa linashikiliwa na wanamgambo hao baada ya serikali iliyoteuliwa na waziri mkuu Mohamed Abdullahi Mohamed kupiga hatua katika masuala ya usalama mjini Moghadishu tangu mwezi Novemba mwaka huu. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)