Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID inaendelea kuhakikisha usalama Khor Abeche Darfur

UNAMID inaendelea kuhakikisha usalama Khor Abeche Darfur

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID umesema unaendelea kushika doria na kuhakikisha usalama wa wakimbizi wa ndani katika mji wa Khor Abeche kwenye jimbo la Darfur.

Mamia ya watu walikimbialia katika eneo la UNAMID kutafuta usalama kufuatia mapigano yaliyozuka wiki iliyopita kati ya jeshi la serikali ya Sudan na kundi la Sudan Liberation Army SLA eneo la Minni Minawi.

Kwa mujibu wa UNAMID wakimbizi wa ndani takribani 1000 wanahifadhiwa katika makao hayo ya UNAMID na imesema wakimbizi wengine wapatao 2000 wamekimbilia eneo la Shangil Tobaya Kaskazini mwa Darfur huku 300 wakielekea Menawashi kilometa 35 mashariki mwa Khor Abeche. UNAMIDI inasema imeongeza doria katika vijiji 34 na makambi ya wakimbizi wa ndani ili kuhakikisha usalama.