Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za Binadamu zinaendelea kukiukwa Ivory Coast:Pillay

Haki za Binadamu zinaendelea kukiukwa Ivory Coast:Pillay

Wakati huohuo Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema anahofia sana ongezeko kubwa la ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast.

Amesema watu zaidi ya 50 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa katika siku tatu zilizopita akiongeza kuwa atahakikisha wanaotekeleza uovu huo wanachukuliwa hatua dhidi ya vitendo vyao.

Bi Pillay amesema wakati watu wanakuwa wahanga wa mauaji ya kukiuka sheria lazima kuwe na uchunguzi na lazima watu wawajibishwe. Ametoa wito kwa pande zote husika kuheshimu haki za binadamu kwa Waivory Coast wote bila ubaguzi.

Amesema ofisi ya haki za binadamu nchini Ivory Coast iko katika tahadhari na itaendelea kuangalia kwa karibu hali nchini humo. Bwana Ibrahim Wani ni mkuu wa ktengo cha Afrika kwenye ofisi ya kamishana mkuu wa haki za binadamu.

(SAUTI YA IBRAHIM WANI)