Kuna ongezeko kubwa la Wakristo wa Iraq wanaokimbia: UNHCR

Kuna ongezeko kubwa la Wakristo wa Iraq wanaokimbia: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuna ongezeko kubwa la Wakristo nchini Iraq kuzikimbia nyumba zao na kwenda katika nchi jirani.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)

UNHCR wakati huohu imeelezea hofu yake juu ya serikali ya Sweden kuwarejesha kwa nguvu Wairaq 20 waomba hifadhi mapema wiki hii. Shirika hilo limeziomba nchi kuwapa waomba hifadhi wa Iraq ulinzi wa kimataifa na kutowarejesha kwa nguvu makundi ya walio wachache au wanaotoka katika maeneo yasiyo na usalama.