Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya mihadarati Afrika ya Magharibi na UNODC

Vita dhidi ya mihadarati Afrika ya Magharibi na UNODC

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kudhibiti madawa ya kulevya( UNODC)umezindua mkakati maalumu kwa ajili ya kukabiliana na ongezeko la madawa ya kulevya katika eneo la Afrika magharibi.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la usafirishwaji wa madawa ya kulevya katika eneo hilo,jambo ambalo pia limechochea kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu. Mpango huo wa Umoja wa Mataifa wa miaka mitano kuanzia mwaka huu 2010 hadi 214 unazihusisha nchi 14 ambazo zitalazimika kushirikiano kukabiliana na wimbo hilo la madawa ya kulevya.

Nchi hizo zote zimeafikia kuweka mikakati ya kiknda ambayo itafanya kazi katika kila nchini.

Katika kufanikisha mkakati huo Umoja wa Mataifa unashirikiana na mamalaka kwenye eneo hilo.