Ajenda za jinsia zishirikishwe kwenye mkutano wa mazingira:UNFPA

17 Disemba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu (UNFPA) limeanza kutupa karata yake ya ushawishi kuhakikisha kwamba mkutano ujao wa dunia kuhusu mazingira na maendeleo endelevu haupi kisogo masuala yanayohusu jinsia, afya ya uzazi na masuala mengine yanayoambatana na ongezeko la watu.

Maafisa wa shirika hilo tayari wamekutana na wawakilishi wa mashirika ya kiraia 20 ambao wamejadiliana namna watavyoweza kuboresha ushirikiano na hatimaye kuhakikisha masuala hayo yanapewa kipaumbele kwenye mkutano huo utakaofanyika mwaka 2012.

Mkutano huo uliopewa jina la Rio + 20 ni mwendelezo wa mkutano mwingine kama huo uliofanyika Rio de Janeiro mwaka 1992. Shabaya kubwa ya mkutano huo ujao ni kusaka utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi duniani kwa ajili ya kusukuma mbele shughuli za maendeleo endelevu na namna ya kuzikabili changamoto mtambuka.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter