Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanzisha mpango mpya BNUB kuleta amani Burundi

UM waanzisha mpango mpya BNUB kuleta amani Burundi

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeanzisha oparesheni nchini Burundi kulisaidia taifa hilo la afrika ya kati wakati linapofanya jitihada katika awamu nyingine kuinuka tena baada ya vita vya miongo kadha vya wenyewe kwa wenyewe.

Baraza hilo la wanachama 15 liliipa jukumu ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi BNUB kuisadia serikali katika kuhakikisha kujisimamia kwa idara zake hususan mahakama na bunge , kupambana na ukwepaji wa sheria na kulinda haki za binadamu.

Ofisi hiyo mpya ni moja ya mipango ya hivi punde ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi nchi ambayo maelfu ya watu waliangamia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wahutu na watusi hata kabla ya kujinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1962.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa hata baada ya juhudi za Burundi za kumaliza ghasia, bado uhaba wa chakula , ukosefu wa usalama na ukiukaji wa haki za binadamu bado ni tatizo.