Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinapuuza sheria zake kuhusu matatizo ya uhamiaji: Pillay

Nchi zinapuuza sheria zake kuhusu matatizo ya uhamiaji: Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amesema mkataba wa kimataifa wa kulinda haki za wafanyakazi wahamiaji na familia zao unasalia kuwa wa chini kuridhiwa kati ya miakata ya kimataifa ya haki za binadamu miaka 20 tangu ulipopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Bi Pillay amesema tunafahamu nini kinachotakiwa ili kulinda haki za binadamu za wafanyakazi wahamiaji na familia zao,bila kuangalia hadhi yao, na inafahamika nini kinachohitajika ili kuchagiza sauti, kuwasaidia, kufuata sheria na kulinda mazingira ya wahamiaji., kwani yote yako kwenye mkataba wa wafanyakazi wahamiaji.

Ameongeza kuwa mataifa yanalifahamu hili kwani miaka 20 iliyopita yalikusanyika pamoja na kupitisha mkataba huo. Pillay ameyasema hayo wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji Jumamosi tarehe 18 Desemba. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)