Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wakimbia machafuko Ivory Coast: UNHCR

Maelfu wakimbia machafuko Ivory Coast: UNHCR

Hali ya usalama imeendelea kuwa tata nchini Ivory Coast kufuatia machafuko ya jana Alhamisi mjini Abijan ambapo watu takribani 20 wafuasi wa Alassane Ouatarra waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika purukshani na askari wa usalama.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR maelfu ya watu wanavuka mipaka na kuingia nchi jirani kwa kuhofia usalama wao. Zaidi ya watu 4000 wamekimbilia Liberia na wengine 200 nchini Guinea. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR
(SAUTI YA MELISSA FLEMING)

UNHCR inasema wimbi hilo la wakimbizi sio kubwa sana na hawajatoa taarifa yoyote kwamba wanalengwa.Wengi wao wanahifadhiwa na wenyeji katika vijiji vya mpakani na UNHCR inatoa msaada kwa familia zionazowahifadhi. Shirika hilo linasema hakuna mipango ya mara moja ya kuweka kambi ya dharura kwa ajili ya wakimbizi hao.