Skip to main content

Hakuna muafaka kuhusu almasi za Zimbabwe:UM

Hakuna muafaka kuhusu almasi za Zimbabwe:UM

Hofu imeelezewa kuhusu kutopatikana kwa muafaka kuhusu suala tata la almasi za Zimbabwe chini ya mchakato wa Kimberly , mpango uliowekwa ili kuhakikisha kwamba biashara ya almasi haihusishi madini kutoka maeneo ya vita.

Biashara ya almasi kutoka machimbo ya Marange Mashariki mwa Zimbabwe yamesababisha utata wa kimataifa kufuatia shutma kwamba jeshi lilitumia nguvu kudhibiti machimbo ya almasi 2008.

Wakati wa tukio hilo watu kadhaa waliuawa na maelfu ya wakulima wadogowadogo walilazimika kukimbia.

Mwenyekiti anayeondoka wa mchakato wa Kimberly Boaz Hirsch ameliambia baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwamba lazima muafaka upatikane. Amesema Israel imeweka msukumo mkubwa katika kupata suluhisho la suala la kusafirisha almasi ambazo hazijasafishwa kutoka Marange nchini Zimbabwe.

Anahofia kwamba hakuna muafaka ulioafikiwa wa kusonga mbele na suala hili. Ameongezea kuwa juhudi kukabiliana na changamoto bado zinaendelea, na kama hawatafanikiwa amependekeza kwamba mwenyekiti atakeshika hatamu atafute suluhisho la muda mrefu la suala hili.