Romania kuisaidia kilimo Moldova: FAO

16 Disemba 2010

Serikali ya Romania imetia saini makubaliano ya kwanza kabisa na shirika la chakula na kilimo FAO ya kuisaidia nchi jirani yake Moldova.

Kwa kufanya hivyo Romania inasahau na kufunga mlango wa kuwa nchi mpokeaji wa msaada kwa miaka ya nyuma na kujuchua jukumu la kutoa msaada wa kifedha kwa Moldova.

Fedha zitakazotolewa na Romania takribani dola 695,000 zitatumiwa na FAO kutoa msaada wa kiufundi kwa jamhuri ya Moldova wakati wa sensa yake ya kwanza ya kilimo inayotarajiwa kufanyika mapema mwakani 2011.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter