Baraza la usalama lamaliza vikwazo na kukumbatia demokrasia Iraq

15 Disemba 2010

Mpango wa mafuta kwa chakula unaoendeshwa na Umoja wa Mataifa kufuatia vikwazo baada ya uvamizi wa Iraq nchini Kuwait mwaka 1990 umehitimishwa rasmi.

Mpango huo ulianzishwa na umoja wa Mataifa kuiruhusu Iraq kuuza mafuta yake ili kununua chakula, madawa na kupunguza adha zinazowakabili Wairaq wa kawaida kutokana na vikwazo ivyowekewa nchi hiyo.  Baraza la usalama likishuhudiwa na makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden limepitisha maazimio matatu ya kumaliza vikwazo vilivyosalia dhidi ya Iraq.

Baraza limesisitiza kwamba linajikita na wajibu wake wa kuhakikisha uhuru, utaifa na umoja, na hadhi ya mipaka ya Iraq inalindwa. Pia limesisitiza umuhimu wa kuwepo usalama na utulivu wa Iraq kwa ajili ya watu wa taifa hilo, kanda nzima na jumuiya ya kimataifa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter